Benki ya kiislamu ya Amana Tanzania inayotoa huduma zake za fedha kwa kufuata misingi ya sheria ya dini ya kiislamu ambayo imeasisiwa na Qur'an pamoja na sunnah ya mtume (swalla llahu a'laihi wasallam). Imefanya semini juu ya mchango wa benki za kiislamu Tanzania na dunia kwa ujumla.
Pia ameelezea huduma zao wanazozitoa kwa wateja wao kama vile akaunti maalum ya hijja, akaunti ya mwanafunzi ambayo iliwavutia wanafunzi wa chuo hicho. Katika semina hiyo wanafunzi washiriki kutoka fani mbali mbali walipata fursa ya kuuliza maswali yaliyokuwa yakiwatanza kwa muda mrefu na kupata majibu ya papo kwa papo.
Wanafunzi ambao wanasoma fani ya Islamic Bank wamesema kwamba wamefurahi sana kupata ujio huo kwasababu ndio semina yao ya kwanza tangu kuanzishwa kwa fani hiyo katika chuo hicho.
Allah awabarik Amana Bank kwa kuonesha mashirikiano mazuri na Zanzibar University.
No comments:
Post a Comment