Kituo cha huduma rafiki kwa vijana (#TAYI) kimewasaidia vijana baada ya kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha, elimu ya uongozi, mitandao ya kijamii pamoja na elimu ya ujasiriamali. Mafunzo hayo yameendeshwa katika mwezi huu wa ramadhani kwa lengo la kuwajenga vijana uwezo.
Vijana wamepata nafasi ya kujifunza mambo mengi sana kama vile maadili ya uongozi na kiongozi bora, kujitambua, na njia za kubuni mawazo ya biashara na miradi yenye kutekelezeka. Katika mawazo ya biashara ambayo yaliibuka kutoka kwa vijana hao ni kilimo cha mboga mboga, ushonaji na ufumaji, ufugaji wa samaki n.k.
Changamoto kubwa zilizojitokeza katika mafunzo hayo ambazo ziliwasilishwa na wanafunzi ni kukosekana kwa vifaa vya kutosha vya kufundishia kama vile computer ambazo zilitumika kwa kiasi kikubwa kufundishia elimu ya mitandao ya kijamii, kukosekana kwa huduma ya Internet yenye nguvu, huduma ya vyoo, kukosekana kwa soko la kuuzia bidhaa amabazo zinatengenezwa kituoni hapo.
Vijana hao wanomba wadau mbali mbali kuweza kujitokeza na kuwasaidia ili waweze kutimiza malengo yao.
No comments:
Post a Comment